Numbers 28:5-8

5 akila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa
Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.
ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini
Robo ya hini ni sawa na lita moja.
ya mafuta ya zeituni.
6 dHii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 7 eSadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu. 8 fAndaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

Sadaka Za Sabato

Copyright information for SwhKC